Daniel 9:11-16

11

aIsraeli yote imekosea sheria yako na kugeuka mbali, nao wamekataa kukutii.

“Kwa hiyo laana na viapo vya hukumu vilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtumishi wa Mungu, vimemiminwa juu yetu, kwa sababu tumefanya dhambi dhidi yako.

12

bUmetimiza maneno uliyosema dhidi yetu na dhidi ya watawala wetu, kwa kuleta maafa makubwa juu yetu. Chini ya mbingu yote kamwe hapajatendeka kitu kama kile kilichotendeka kwa Yerusalemu.

13

cKama vile ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, misiba hii yote imekuja juu yetu, lakini hatujaomba fadhili kwa Bwana Mwenyezi Mungu wetu kwa kugeuka kutoka dhambi zetu na kuwa wasikivu katika kweli yake.

14

d Bwana hakusita kuleta maafa juu yetu, kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu wetu ni mwenye haki katika kila afanyalo; lakini hata hivyo hatujamtii.

15 e“Sasa, Ee Bwana Mungu wetu, ambaye uliwatoa watu wako Misri kwa mkono wenye nguvu, na ambaye umejifanyia Jina linalodumu mpaka leo, tumetenda dhambi, tumefanya mabaya. 16 fEe Bwana, wewe kwa kadiri ya matendo yako ya haki, ondoa hasira yako na ghadhabu yako juu ya Yerusalemu, mji wako, mlima wako mtakatifu. Dhambi zetu na maovu ya baba zetu yameifanya Yerusalemu na watu wako kitu cha kudharauliwa kwa wale wote wanaotuzunguka.

Copyright information for SwhKC